IQNA

Katika Picha: Maelfu washiriki Hauli ya 35 ya Kuaga Dunia Imam Khomeini

IQNA - Maelfu ya watu walikusanyika katika kaburi la Imam Khomeini, kusini mwa Tehran, tarehe 3 Juni, 2024, ili kumuenzi marehemu muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu na kutangaza upya utiifu kwa malengo yake matukufu. Hauli hiyo ilihutubiwa na Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Miaka 35 iliyopita, Imam Ruhullah Musawi Khomeini (MA) mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 87. Ulimwengu wa Kiislamu uligubikwa na majonzi na huzuni kubwa kuutokana na kutangazwa kifo cha Imam. Alianza kujishughulisha na siasa sambamba na masuala ya kielimu na kiutamaduni. Mapambano ya Imam dhidi ya utawala wa Shah na uingiliaji wa Marekani nchini Iran yalishtadi mwaka 1963  na kupelekea Imam kubaidishwa kwa miaka 13 nchini Iraq, Uturuki na Ufaransa. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipata ushindi mwaka 1979 kwa uongozi shupavu wa Imam Khomeini (MA).