Kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, ubainishaji wa aina zote za hisia unapaswa kuwa na uhusiano na Mwenyezi Mungu na mapenzi yake. Hii ni kweli kuhusu hisia hasi kama vile hofu pia. Ili kufikia nidhamu ya kihisia, mtu lazima ajiondoe katika udhibiti au mamlaka ya Shetani ili aweze kuwa huru kutokana na hofu ambayo Shetani anaiingiza moyoni mwake. Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 175 ya Surah Al Imran: “Hakika huyo ni Shetani anawatia hofu marafiki zake, basi msiwaogope (maadui), bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini."
Kimsingi, Shetani huendeleza mambo yake na kuwafanya watu wafanye mambo mabaya kwa kuwatisha kwa umaskini na taabu. “Shet'ani anakutieni hofu ya ufakiri na anakuamrisheni mambo machafu. Na Mwenyezi Mungu anakuahidini msamaha na fadhila zitokazo kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.” (Aya ya 268 ya Surah Al-Baqarah).
3488031
Kujiweka huru kutoka kwa Shetani ni mwanzo wa kupata uhuru kutoka kuwa na hofu ya mtu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kupata uhuru na uwezo ni kupitia tu imani katika Mungu. Ndio maana Mwenyezi Mungu ameharamisha khofu yoyote isipokuwa Khashia Yake: “Je, hamtapigana na watu walio vunja viapo vyao na wakawa na hamu ya kumfukuza Mtume, nao ndio walio kuanzeni mara ya kwanza? Je, mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini." (Aya ya 13 ya Surah At-Tawbah)
Mwenyezi Mungu pia anatuamuru tuepuke kuogopa watu. Ikirejelea hofu ya watu kwa baadhi ya wanavyuoni wa Kiyahudi, Qur'ani Tukufu inasema: “Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walio nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na wanazuoni, waliwahukumu Mayahudi; kwani walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nao wakawa ni mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache. Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri." (Aya ya 44 ya Surah Al-Ma’idah)
Kimsingi, kuzingatia yale wengine wanafikiri na kuogopa kile wanachoweza kusema yamkini kukamfanya mtu kuchanganyikiwa na kutokuwa na lengo, kudhoofisha uwezo wake wa mawazo na busara, na kumpeleka kwenye kuchanganyikiwa. Kumcha Mungu, kwa upande mwingine, humsaidia mtu kuwa huru na mtiifu kwa Muumba pekee na Msimamizi wa ulimwengu na hali hiyo humuondolea mja hofu na unyonge wote.