IQNA

Qur'ani Tukufu

Siku ya Kimataifa ya Qur'ani yaadhimishwa huko Iraq

23:04 - February 11, 2025
Habari ID: 3480196
IQNA-Darul Quran ya Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS) imetangaza kumalizika kwa programu za Siku ya Kimataifa ya Qur'an baada ya ushiriki mkubwa wa vikundi vya ndani na kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa.programu za hafla hii zilidumu kwa zaidi ya wiki moja na zilihusisha mikutano na shughuli za Qur'an pamoja na shindano la Mahdi lililokuwa na ushiriki wa kimataifa.

Sayyid Ibrahim Al-Mousawi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Kimataifa ya Qur'an ya Iraq, alipongeza jitihada za vikundi vilivyoshiriki kutoka ndani na nje ya Iraq katika hafla hii na kusema: watafiti na wasomaji maarufu kutoka nchi 12 za Kiarabu na Kiislamu walishiriki katika hafla hizi na watafiti 170 kutoka Syria, Lebanon, Misri, Iran, Algeria, Ufaransa, Uingereza na Iraq walikuwa miongoni mwa washiriki wa Mkutano wa Sita wa Kimataifa wa Imam Hussein (AS).

Aliongeza: Mkutano huu ulikuwa fursa ya kubadilishana maoni kuhusu fikra za Qur'ani na kufafanua mchango wa Ahlul Bayt (AS) katika ujenzi wa ustaarabu wa Kiislamu.

Al-Mousawi pia alisema: Uzinduzi wa Ensiklopedia ya Qur'an ya Ahlul Bayt (AS) baada ya zaidi ya miaka 10 ya juhudi za utafiti endelevu na kuzindua mpango wa kitaifa wa kutambua na kukuza uwezo wa Qur'an mpya wa vikundi vya umri mbalimbali ulikuwa miongoni mwa programu za Siku ya Kimataifa ya Qur'an.

Alibainisha: Zaidi ya mikutano ya Qur'ani ipatayo 23 ilifanyika katika majimbo 16 ya Iraq ambayo yalikuwa na jukumu kubwa katika kusambaza ujumbe wa Qur'ani na kuimarisha utamaduni wa Qur'ani miongoni mwa vikundi mbalimbali vya jamii.

Al-Mousawi alisisitiza: Darul Quran ya Haram Takatifu ya Husseini ina mipango ya kuimarisha miradi yake ya Qur'ani kwa siku zijazo kwa lengo la kusambaza fikra za Qur'ani na kuimarisha uhusiano na vikundi mbalimbali vya kitamaduni na matokeo yaliyopatikana kutokana na programu za Qur'an ni hatua muhimu kwa ajili ya kuendeleza na kuboresha shughuli hizi.

Kwa mujibu wa taarifa hii, programu za Siku ya Kimataifa ya Qur’ani nchini Iraq ambazo zilianza kwa mnasaba wa Siku ya Mab'ath zilivutia wengi hasa katika mitandao ya kijamii duniani kote ambapo zaidi ya wasomaji Qur’ani maarufu wapato 50 kutoka Ulimwengu wa Kiislamu walishiriki.

4265430

Kishikizo: qurani tukufu
captcha