IQNA

Kongamano la ‘Nafasi ya Mwanamke Muislamu Katika Malezi’ kufanyika Zambia

14:10 - May 18, 2009
Habari ID: 1779621
Kongamano wa ‘Nafasi ya Mwanamke Muislamu Katika Malezi ya Watoto’ litafanyika mwezi ujao wa Juni nchini Zambia.
Kwa mujibu wa mwambata wa utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kongamano hilo litafanyika katika ukumbi wa Imam Reza (AS) mjini Lusaka.
Kongamano hilo litajumuisha mihadhara ya wasomi na Maulamaa pamoja na mashindano ya kiutamaduni yatakayokuwa na maudhui zinazohusiana na maisha ya kisiasa, kijamuu na kimalezi ya Bibi Fatima Zahra (AS). Vijana na watu wazima wanatazamiwa kushiriki katika kongamano hilo ambalo litafanyika kwa munasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Bibi Fatima Zahra (AS) ambayo huadhimishwa kama ‘Siku ya Wanawake’.
Kati ya shughuli zingine zilizopangwa siku hiyo ni kuchapishwa makala yenye anuani ya ‘Haki za Mwanamke Katika Uislamu’ katika gazeti la kila siku la Daily Mail la Zambia. Siku hiyo pia kumeandaliwa mdahalo katika radio na mada itakuwa ‘Mafanikio ya Wanawake katika Mapinduzi ya Kiislamu’ . Mwambata wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Zambia ameongeza kuwa kutafanyika pia hafla ya kuadhimisha kuzaliwa Bibi Fatima Zahra (AS) katika kituo cha utamaduni cha eneo la Kutuba na mji wa Livingstone. 405919
captcha