Shirika la habari la Associated Press of Pakistan limeripoti kuwa semina hiyo itakayosimamiwa na Kitengo cha Utafiti wa Kiislamu na Kiarabu cha Chuo Kikuu cha Iqbal itahutubiwa na msomi mashuhuri wa Pakistan Ishfaq Hussein na Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iqbal Nazir Ahmad.
Semina hiyo itahudhuriwa na wanachuo, wataalamu wa taasisi mbalimbali za elimu na wawakilishi wa vyuo vikuu kutoka maeneo yote ya Pakistan.
Wahadhiri kadhaa wa Chuo Kikuu cha Allamah Iqbal Lahore pia watahutubia katika semina hiyo. 783456