IQNA

Yamkini Waziri Mkuu wa Israel ameambukizwa corona

22:15 - March 30, 2020
Habari ID: 3472617
TEHRAN (IQNA) - Kuna uwezekano Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameambukizwa ugonjwa hatari wa COVID-19 au corona baada ya vipimo vya mshauri wake wa karibu kuonesha amekumbwa na maradhi hayo yanayoenenea kwa kasi duniani

Tovuti ya elnashra.com imeandika kuwa, vipimo vya Rivka Paluch, mshauri wa karibu wa Benjamin Netanyahu vinaonesha kuwa mshauri huyo amekumbwa na kirusi cha corona, masaa machache baada ya mumewe kulazwa hospitalini kutokana na ugonjwa huo hatari. Duru moja katika ofisi ya Benjamin Netanyahu ameiambia kanali ya 12 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni kwamba wao wanatekeleza amri na muongozo wa wizara ya afya kwa maana kwamba Netanyahu na washauri wake pamoja na wabunge wa utawala wa Kizayuni watalazimika kuwekwa chini ya karantini kwa muda wa wiki mbili.

Taarifa zinasema kuwa, siku ya Alkhamisi, mshauri huyo wa Netanyahu alishiriki katika kikao cha bunge la Knesset kilichomchagua Jenerali Benny Gantz kuwa spika wa bunge hilo ambapo mbali na kuonana kwa karibu na wabunge wa Israel, alifanya mazungumzo ya karibu pia na washauri na maafisa wengine wa ngazi za juu wa utawala wa Kizayuni. Siku ya Alkhamisi pia, Rivka Paluch alionana na Benjamin Netanyahu, suala ambalo limezidi kupandisha juu uwezekano kwamba waziri mkuu huyo wa utawala wa Kizayuni naye amekumbwa na janga la corona.

Baraza la Mawaziri la Israel limepasisha sheria ya kupiga marufuku mikusanyiko ya zaidi ya watu 10 na pia kuchunga masafa ya mita mbili baina ya mtu na mtu. Maelfu ya wakazi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameshaambukizwa corona hadi hivi sasa.

Hadi sasa watu wapatao 4,695 wameambukizwa corona katika utawala wa Isarel ambapo 16 miongoni mwao wamefariki.

888139

captcha