IQNA

TEHRAN (IQNA) – Qiraa ya hivi karibuni ya Qarii mashuhuri wa Qur'ani Tukufu kutoka Misri Sheikh Ahmad Ahmad Al Nuaina aliposoma aya katika Sura za A-Duha na Al-Inshirah.

Sheikh Daktari Nuaina ni qariii mtajika Misri na amepata umashuhuri kutokana na mbinu kumi tafauti anazotumia kusoma Qur'ani Tukufu.

Qarii huyu mashuhuri wa Misri amewahi kusoma katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Misri na nchi nyingi za Kiislamu. Mbali na kuwa msomaji wa Qur'ani pia amehifadhi kikamilifu kitabu hicho kitukufu. Taaluma nyingine ya Sheikh Nuaina ni daktari wa watoto.

3909116