IQNA

18:52 - July 11, 2020
Habari ID: 3472951
TEHRAN (IQNA) – Qiraa ya qarii maarufu wa Misri marhum Sheikh Sayed Mutawalli Abdul Aal katika mji wa Tabriz, Iran imesambazwa katika mitandao ya intaneti hivi karibuni.

Klipu hii ya video ilirekodiwa Februari 2001 wakati qarii huyu bingwa wa Misri alipoutembelea mji huo wa kaskazini magharibi mwa Iran.

Sheikh Sayed Mutawalli Abdul Aal alizaliwa Aprili 1947 katika familia ya wacha Mngu nchini Misri ambapo aliweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12.

Alianza kujifunza qiraa ya Qur'ani Tukufu kwa kuiga mitindo ya maustadhi bingwa kama vile Sheikh Abdulbasit Abduswamad na Sheilh Mustafa Ismail.

Katika umri wake uliojaa baraka za Qur'ani, Sheikh Sayed Mutawalli Abdul Aal aliweza kutembelea nchi nyingi duniani kama qarii na pia jaji wa mashindano ya Qur'ani. Alifariki Julai 16, 2015 akiwa na umri wa miaka 68.

3909394

Kishikizo: iran ، qarii ، misri ، Mutawalli ، qurani tukufu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: