IQNA

Kongamano la 34 la Umoja wa Kiislamu, Jitihada ya kuleta umoja katika umma

TEHRAN (IQNA)- Kongamano la 35 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu lilianza Jumanne hapa mjini Tehran na litaendelea kwa muda wa siku tano ambapo wasomi, maulamaa na wanazuoni kutoka nchi Zaidi ya 16 wanahutubu kuhusu masuala mbali mbali ya Umma wa Kiislamu.

Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo, mbali na Rais Ebrahim Raisi wa Iran, shakhsia wengine waliohutubu ni pamoja na Ziyad Nakhalah, Katibu Mkuu wa Jihadul-Islami ya Palestina, waziri mkuu wa zamani wa Iraq Adil al-Mahdi, Mufti wa Croatia Aziz Hasanvich, Mkuu wa masuala ya kimataifa wa Harakati ya Hamas Khalil al Hillah, Spika wa bunge la Algeria Bou Abdullah Bou Ghulamullah na wanafikra wengine kadhaa wa Ulimwengu wa Kiislamu.