IQNA

Hamas: Mapambano ni chaguo bora zaidi la kuikomboa Palestina

17:31 - October 20, 2021
Habari ID: 3474447
TEHRAN (IQNA)- Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), amesema muqawama au mapambano ndio njia bora zaidi ya kukomboa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ismail Ridhwan amesema utawala wa Kizayuni wa Israel unafahamu tu lugha la mabavu na kuongeza kuwa, “tunaamini kuwa chaguo bora zaidi linaloweza kutumika kukomboa ardhi zote za Palestina ni mapambano.”

Ridhwan ametahadharisha kuhusu hatari inayoukabili mji wa Quds (Jerusalem) na Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji huo na kubaini kuwa hatari hiyo ni kutoka kwa Wazayuni maghasibu wanaopata himaya ya Marekani na pia mikataba ya baadhi ya tawala kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel. Amesema lengo kuu la utawala wa Kizayuni ni kuubomoa msikiti wa Al Aqsa na kujenga hekalu la Kizayuni mahala pake.

Afisa huyo wa Hamas amesisitiza  kuwa njia bora zaidi ya kukabiliana na njama hizo ni kuwepo umoja wa Waarabu na Waislamu wote duniani katika kuunga mkono harakati za mapambano ya Wapalestina.

Amesisitiza kuhusu umuhimu wa mji wa Quds kwa Waislamu duaniani na kusema msikit wa Al Aqsa mjini humo ni qibla cha kwanza cha Waislamu na ni sehemu ambaki kulijiri kisa cha Israa na  Mi’raj ya Mtume Muhammad SAW.

Aidha amesema kadhia ya Quds ni kadhia ya umma wote wa Waislamu na kuongeza kuwa, umoja ndio nguvu ya Umma wa Kiislamu na ni kupitia umoja ndio Waislamu wataweza kukabiliana na matatizo waliyonayo leo.

Mkutano wa 35 wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza leo hapa mjini Tehran kwa mnasaba wa kuanza Wiki ya Umoja, chini ya kaulimbiu ya "Umoja wa Kiislamu; Amani na Kuepukana na Mifarakano."

Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo, mbali na Rais Ebrahim Raisi, shakhsia wengine waliohutubu ni pamoja na Ziyad Nakhalah, Katibu Mkuu wa Jihadul-Islami ya Palestina, waziri mkuu wa zamani wa Iraq Adil al-Mahdi, Mufti wa Croatia Aziz Hasanvich, Mkuu wa masuala ya kimataifa wa Harakati ya Hamas Khalil al Hillah, Spika wa bunge la Algeria Bou Abdullah Bou Ghulamullah na wanafikra wengine kadhaa wa Ulimwengu wa Kiislamu.

4006483

 

captcha