IQNA

Siku ya Kimataifa ya Kuonyesha Mshikamano na Taifa la Palestina

15:34 - November 29, 2021
Habari ID: 3474616
TEHRAN (IQNA)- Leo tarehe 29 Novemba inaadhimishwa kote duniani kama Siku ya Kimataifa ya Kuonesha Mshikamano na Taifa la Palestina

Mwaka 1977 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliitangaza Tarehe 29 Novemba kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Kuonesha Mshikamano na Taifa la Palestina. Sababu ya hatua huyo ya Umoja wa Mataifa ni nafasi na mchango wa Baraza Kuu la umoja huo katika kuigawa ardhi ya Palestina. Tarehe 29 Novemba 1947 baraza hilo lilipasisha azimio nambari 181 lililoidhinisha kugawanywa ardhi ya Palestina. Kwa mujibu wa azimio hilo Palestina iligawanywa sehemu mbili kwa ajili ya kuundwa dola la Kiyahudi na nchi ya Palestina. Pamoja na hayo hadi sasa utawala ghasibu wa Israel haujawahi kuheshimu azimio hilo na daima umekuwa ukijitanua na kutwaa ardhi zaidi za Palestina kwa kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi iliyoghusubiwa.

Tabia hiyo ya Israel ya kutoheshimu azimio nambari 181 ilikuwa sababu ya Baraza Kuu kuchukua uamuzi wa kuitangaza tarehe 29 Novemba kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Kuonesha Mshikamano na Taifa la Palestina ili angalau iwapoze Wapalestina kwa njia moja au nyingine. Hata hivyo tunaweza kusema kuwa, kutangazwa siku hiyo hakujawa na taathira yoyote katika hali ya Palestina licha ya kupita miaka 42 sasa.  Hii ni kwa sababu madola makubwa yenye kura ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, yaani Uingereza na Marekani yamekuwa yakizuia hatua zozote kuchukuliwa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendeleza jinai dhidi ya watu wa Palestina.

3476707

captcha