IQNA

Ragheb Mustafa Ghalwash, bingwa katika sauti ya usomaji Qur'ani Tukufu

TEHRAN (IQNA)- Ragheb Mustafa Ghalwash alikuwa mmoja kati ya wasomaji bora zaidi wa Qur'ai nchini Misri na ametajwa kuwa qarii kijana zaidi wakati wa 'zama za dhahabu' katika qiraa ya Qur'ani Tukufu nchini Misri.

Sheikh Ragheb Mustafa Ghalwash  alizaliwa Julai 5 mwaka 1938 nchini Misri na kukulia katika familia iliyokuwa na mapenzi makubwa na Qur'ani. Raghib Mustafa Ghalwash alikuwa tayari amehifadhi Qur'ani nzima katika rika la barobaro na kuanza kusoma kitabu hicho katika hafali na majlisi mbalimbali akiwa na umri wa miaka 16.

Alijiunga na Radio ya Qur'ani Misri ambapo alipata umashuhuri mkubwa wakati huo akisoma pamoja na magiwji wengine wa qiraa ya Qur'ani Tukufu kama vile Mustafa Ismail, Abdul Basit Abdul Samad, Mahmoud Khalil al-Husari na wengine.

Sheikh Raghib Mustafa Ghalwash alikuwa miongoni mwa wasomaji wa Qur'ani waliofanya safari nchini Iran baada ya kumalizika vita vya kulazimishwa vilivyoanzisha na Iraq dhidi ya Iran. Sheikh Ghalwash aliaga dunia Februari 4 mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 78 uliojaa baraka.

Qiraa na kisomo cha gwiji huyo wa Misri kilipendwa sana nchini Iran na maeneo mengine ya ulimwengu wa Kiislamu.

Sheikh Ghalwash alitembelea Iran nyakati tafauti kuanzia mwaka 1989 hadi 2000 na katika moja ya safari zake hizo alipata fursa ya kusoma Qur’ani Tukufu katika kikao kilichohudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei.

Hapa chini ni klipu ya historia fupi na qiraa ya Marhum Sheikh Ghalwash

4032749

Kishikizo: qurani tukufu ، ghalwash ، iran