IQNA

Qiraa ya marhum Sheikh Ghalwash mbele ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

22:37 - November 17, 2020
Habari ID: 3473369
TEHRAN (IQNA) – Qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Mustafa Ghalwash katika moja ya safari zake nchini Iran alisoma Qur’ani Tukufu mbele ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Sheikh Ragheb Mustafa Ghalwash aliaga dunia Februari 4 mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 77 uliojaa baraka.

Ghalwash alizaliwa Julai 5 mwaka 1938 nchini Misri na kukulia katika familia iliyokuwa na mapenzi makubwa na Qur'ani. Raghib Mustafa Ghalwash alikuwa tayari amehifadhi Qur'ani nzima katika rika la ubalobaro na kuanza kusoma kitabu hicho katika hafali na majlisi mbalimbali akiwa na umri wa miaka 16. Sheikh Raghib Mustafa Ghalwash alikuwa miongoni mwa wasomaji wa Qur'ani waliofanya safari nchini Iran baada ya kumalizika vita vya kulazimishwa vilivyoanzisha na Iraq dhidi ya Iran. Qiraa na kisomo cha gwiji huyo wa Misri kilipendwa sana nchini Iran. 

Sheikh Ghalwash alitembelea Iran nyakati tafauti kuanzia mwaka 1989 hadi 2000 na katika moja ya safari zake hizo alipata fursa ya kusoma Qur’ani Tukufu katika kikao kilichohudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei.

Katika klipu hii hapa chini, Sheikh Ghalwash anasoma sehemu ya Sura Maryam mwaka 1989,  katika kikao kilichohudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Tehran.

3935774

captcha