Akizungumza na IQNA, Savadkouhi amesema, “Qur’ani ni nuru ambayo, inapomwingia mtu, hufanya kila kitu kuwa wazi zaidi na chenye maana kubwa.”
Amesisitiza kuwa manufaa ya kiroho na kiakili ya kuhifadhi Qur’ani yanaenda mbali zaidi ya ibada ya kidini pekee.
Akielezea uzoefu wake, alisema, “Daima nimehisi athari chanya za Qur’anim kwenye ustawi wa wangi wa kiakili, kwenye matendo yangu, na hata wakati wa mitihani ya kuingia chuo kikuu.”
Ingawa kuhifadhi Qur’ani hakupi upendeleo maalum katika tathmini za kitaifa za kitaaluma nchini Iran, alibainisha kuwa manufaa yake kwa uwezo wa kiakili hayawezi kupuuzwa.
“Hakuna upendeleo kwa wahifadhi wa Qur’ani katika mitihani ya kuingia chuo kikuu, lakini kuwa na uhusiano na Qur’ani, hasa katika masomo kama elimu ya dini na Kiarabu, kuliisaidia sana akili yangu. “Qur;ani imeimarisha umakini wangu na ukali wa fikra,” aliongeza.
Savadkouhi alianza safari yake ya kuhifadhi Qur’ani miaka kadhaa iliyopita, akitumia miaka mitatu hadi mitano kuhifadhi Juzuu 20.
3493198