IQNA

Shule ya Kitaifa ya Weledi wa Qiraa ya Qur'ani imezinduliwa Tehran

19:01 - May 03, 2025
Habari ID: 3480629
IQNA – Katika sherehe iliyofanyika Tehran Alhamisi, Shule ya Kitaifa ya Weledi wa Qiraa ya Qur'ani ilizinduliwa.

Sherehe hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Eram, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Shirika la Waqfu na Masuala ya Sadaka, Hujjatul Islam Seyed Mehdi Khamoushi, pamoja na watu mashuhuri wa Kiislamu nchini Iran, wakiwemo wataalamu na wasomi wa Qur'ani.

Baada ya kusomwa kwa aya za Qur'ani Tukufu na Qari mchanga, Sobhan Abdollahi, mtendaji mkongwe wa masuala ya Qur'ani, Abbas Salimi, alipanda jukwaani na kusema kuwa mustakabali wa nchi unategemea vijana na watoto, na kwamba ikiwa watafungamana na Qur'ani, wanaweza kuhakikisha mustakabali mzuri kwa nchi yao.

Aliashiria Hadithi inayohusiana na umuhimu wa elimu utotoni na kusema, "Je, ni nini bora zaidi kuliko neno na kitabu cha Mungu kwa elimu?"
Akiongeza kuwa uzinduzi wa Shule ya Kitaifa ya Weledi wa Qiraa ya Qur'ani ni hatua nzuri na ya thamani, alisema hatua hii ya kudumu ilichukuliwa kwa msaada wa mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu na mkuu wa Shirika la Waqfu la Iran.

"Nina hakika kwamba mfano huu, kwa ushiriki na msaada wa watu wema, unaweza kuwa mfano kwa nchi zote za Kiislamu," alisema.

Ali Mehrabi, mkuu wa shule hiyo, pia alielezea shughuli za shule hiyo, akisema kwamba Shule ya Kitaifa ya Weledi wa Qiraa ya Qur'ani itafanya kazi katika maeneo matatu.
"Eneo la kwanza na linalolengwa ni la qiraa ikiwemo Tarteel, kuhifadhi kwa kuzingatia maudhi, na qiraa ya kuiga. La pili ni ufanisi wa qiraa ya Qur'ani na la tatu ni elimu ya Qur'ani. Katika maeneo haya yote, mahitaji ya kielimu na kisaikolojia yatazingatiwa."

 

3492901

Habari zinazohusiana
Kishikizo: iran qurani tukufu
captcha