IQNA

Ibada ya Hija

Qarii wa Iran akisoma Surah Baqarah katika Masjid al-Haram mjini Makka

TEHRAN (IQNA)- Qarii wa Kimataifa wa Qur'ani Tukufu Ustadh Yousef Jafarzadeh hivi karibuni alisoma aya ya 125 ya Surah Baqarah katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, Al Masjidul Haram.
Ustadh Jafarzadeh ni mwanachama wa Msafara wa Qur'ani wa Nur ambao umetumwa Makka na Madina katika msimu huu wa Hija kwa lengo la kustawisha na kuhimiza usomaji Qur'ani Tukufu.