makka

IQNA

IQNA – Ziara ya siku mbili ya kukagua vituo vya afya katika mji mtukufu wa Makka, ili kutathmini utayari wao kwa msimu ujao wa Hija, imekamilishwa na waziri wa afya wa Saudia.
Habari ID: 3482160    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/25

IQNA – Msahafu au nakala ya Qur’ani, iliyondikwa kwa mkono nchini India katika karne ya 19, imepelekwa kwenye maonyesho ya Makumbusho ya Qur’ani Tukufu katika eneo la utamaduni la Hira katika mji mtakatifu wa Makka.
Habari ID: 3482156    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/21

IQNA – Matengenezo ya Al‑Kaaba Tukufu pamoja na Hijr Ismail yamekamilika kwa kufuata viwango vya juu vya kihandisi na kiufundi.
Habari ID: 3482153    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/19

IQNA – Bahari kubwa ya waumini ilijaza Msikiti Mtukufu wa Makka (Masjid al-Haram) siku ya Ijumaa, walipokusanyika kwa ajili ya swala ya Ijumaa ya kwanza katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3481965    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/21

IQNA – Uendelezaji wa Kijiji cha Hija cha Indonesia mjini Makkah ni mhimili mkuu wa ahadi ya Rais Prabowo Subianto ya kuhakikisha ibada ya Hija inakuwa nafuu zaidi, hatua inayolenga kupunguza mzigo wa kifedha kwa mamilioni ya Waislamu wa Indonesia.
Habari ID: 3481911    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/09

IQNA – Wageni wa Jumba la Makumbusho ya Qur’ani Tukufu katika Wilaya ya Kitamaduni ya Ḥirā’, mjini Makka, sasa wanayo fursa ya kushuhudia turathi adhimu iliyovunja rekodi ya dunia: nakala ya Qur’ani Tukufu iliyoandikwa kwa mkono, iliyo kubwa zaidi kuliko zote duniani, ambayo sasa inaonyeshwa rasmi kwa umma.
Habari ID: 3481893    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/05

IQNA – Nakala ya kihistoria na yenye thamani kubwa ya Qur'ani Tukufu, inayojulikana kama “Qur'ani ya Kufi,” imewekwa wazi kwa umma katika Makumbusho ya Qurani ya Makka.
Habari ID: 3481840    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/24

IQNA – Katika juhudi za kuboresha huduma kwa mahujaji na wakazi wa Makkah, kampuni ya RUA Al Haram Al Makki imetangaza mradi mkubwa wa maendeleo unaojulikana kama Lango la Mfalme Salman , utakaojengwa karibu na Msikiti Mkuu wa Makkah. Mradi huu utaongoza takriban maeneo 900,000 ya kuswali ndani na nje ya jengo.
Habari ID: 3481376    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/17

IQNA – Mamlaka Kuu ya Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu imetangaza mafanikio ya utekelezaji wa mazingira ya kidijitali katika Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume (SAW) mjini Madina.
Habari ID: 3481254    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/19

IQNA – Warsha ya mafunzo kuhusu stadi za msingi za huduma ya kwanza imefanyika kwa wafanyakazi wa Msikiti Mkuu, Masjid Al Haram, ulioko katika mji mtukufu wa Makka.
Habari ID: 3481218    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/12

IQNA – Raundi ya mwisho ya Mashindano ya 45 ya Kimataifa ya Mfalme Abdulaziz ya Kuhifadhi, Kusoma, na Kufasiri Qur’ani Tukufu imemalizika Alhamisi katika Msikiti Mtukufu wa Makkah.
Habari ID: 3481089    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/15

IQNA – Msikiti Mtakatifu jijini Makkah unatarajiwa kuanza kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani kuanzia Jumamosi.
Habari ID: 3481053    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/09

IQNA-Kozi ya kiangazi ya wanawake ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu katika Msikiti Mtukufu wa Masjid al-Haram, Makkah, imekamilika kwa mafanikio, ambapo washiriki zaidi ya 1,600 wametimiza masharti ya programu hiyo.
Habari ID: 3481013    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/28

IQNA – Kozi maalum ya kiangazi ya kuhifadhi na kusoma Qur’ani kwa wanawake imezinduliwa katika Msikiti Mkuu wa Makka maarufu kama Masjid al Haram.
Habari ID: 3480971    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/20

IQNA – Jumanne, tarehe 15 Julai 2025, jua limeonekana moja kwa moja juu ya Al-Kaaba huko Makka, hali itakayowawezesha Waislamu kote duniani kuthibitisha mwelekeo wa Qibla kwa usahihi mkubwa.
Habari ID: 3480945    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/15

IQNA – Msikiti Mtukufu wa Makka uliangaziwa na tukio la kipekee Alhamisi, ambapo shughuli ya kila mwaka ya kuosha Kaaba (Ghusl ya Kaaba) ilitekelezwa kwa heshima na taadhima kubwa.
Habari ID: 3480928    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/11

IQNA – Mamlaka za Saudi Arabia zimeripoti utoaji wa huduma mbalimbali kwa mahujaji na wageni waliotembelea Msikiti Mtukufu wa Makkah katika mwaka wa 1446 na mwanzoni mwa mwaka 1447 Hijria, kama sehemu ya juhudi zinazoendelea kusaidia wasafiri wa kidini na kusimamia shughuli za ibada.
Habari ID: 3480919    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/09

IQNA – Hamada Muhammad al-Sayyid, hafidh wa Qur'ani kutoka Misri, ameshinda nafasi ya kwanza katika mashindano ya kwanza ya kuhifadhi Qur'ani kwa Mahujaji, yaliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Makka
Habari ID: 3480817    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/10

IQNA – Maonesho ya kudumu katika Makumbusho ya Qur'ani jijini Makkah yanawapa wageni tajiriba ya kipekee ya kiutamaduni na kiroho kupitia hati nadra za Qur'ani na nakala kubwa zaidi ya Qur'ani duniani.
Habari ID: 3480811    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/09

IQNA – Jumla ya milango 199 imewezeshwa ili kuboresha mtiririko wa Mahujaji wanaoingia na kutoka katika Msikiti Mkuu wa Makka, Masjid al Haram na Msikiti wa Mtume, Al Masjid an Nabawi, huko Madina wakati wa msimu wa Hija.
Habari ID: 3480768    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/31