IQNA

Msikiti wa al-Zahir Baybars uliojengwa miaka 800 iliyopita Cairo, Misri

Baada ya muongo mmoja na nusu wa kazi ya ukarabati, Msikiti wa kihistoria wa al-Zahir Baybars huko Cairo uliwakaribisha waumini tena mapema Juni 2023.

Msikiti huo, ambao uliojengwa miaka 800 iliyopita na umepewa jina la sultani wa silsila ya watawala wa Mamluk, al-Zahir Baybars al-Bunduqdari, aliyeujenga, ni wa tatu kwa ukubwa nchini Misri. Unajivunia mnara wa kipekee, ua mpana na historia tajiri ya umuhimu wa kidini na kitamaduni.