Siku ya Ashura mjini Witu, Kaunti ya Lamu, Kenya
IQNA-Waislamu wa mji wa Witu katika Kaunti ya Lamu, pwani ya Kenya wameshiriki katika maombolezo ya siku ya Ashura, ambayo ni kumbukumbu ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (SAW), Imam Hussein bin Ali (AS), watu wa nyumba yake na wafuasi wake watiifu katika uwanda wa Karbala, Iraq mwaka 61 Hijria Qamaria. Maadhimisho hayo yameandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Umul Banin mjini humo. Hizi hapa chini klipu za maombolezo hayo.
copied
https://iqna.ir/H0Ebvq