IQNA

Msikiti mkubwa zaidi nchini Djibouti, kwa hisani ya Uturuki

18:52 - November 28, 2019
Habari ID: 3472238
TEHRAN (IQNA) – Miaka mine iliyopita, uliwekwa msingi wa Msikiti wa Abdülhamid II nchini Djibouti na sasa mradi huo umekamilika.

Msikiti huo umejengwa kwa ufadhili wa Wakfu wa Kidini Uturuki (TDV)  na una uwezo wa kubeba waumini 6,000 na hivyo kuufanya kuwa msikiti mkubwa zaidi katika nchi hiyo ya mashariki mwa Afrika.

Msikiti huo una usanifu majengo wa Kiuthmaniya na umepewa jina la mfalme maarufu wa Kiuthmaniya, Sultan Abdülhamid II . Wauthmaniya walikuwa na uhusiano mzuri na eneo la mwambao wa Afrika Mashariki kwa karne nne na serikali ya sasa ya Uturuki imeendeleza uhusiano huo.

Pendekezo la ujenzi wa msikiti huo liliwasilishwa wakati Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki alipoitembelea Djibouti mwaka 2015.  Wakati wa safari hiyo, Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alisema angependa kuuona msikiti wenye usanifu majengo wa Kiuthmaniya na “kusikia adhana kama ile ya Istanbul.”

Msikiti huo ambao umejengwa katika mji mkuu, Mji wa Djibouti uko karibu na ufukwe wa bahari katika mtaa iliko ikulu ya rais.

Msikiti huo una minara miwili yenye urefu wa mita 46 na kuba la mita 27 huku kuta ziwa zina aya za Qur’ani zilizoandikwa kwa kaligrafia ya Kiuthmaniya. Wakfu wa Kidini Uturuki (TDV) , ambao unafungamana na Idara ya Masuala ya Kidini katika Ofisi ya Rais wa Uturuki (DIB) unahusika katika ujenzi wa misikiti Uturuki na maeneo mengine duniani.

3859658

captcha