msikiti

IQNA

IQNA – Rais wa msikiti mmoja mjini Milwaukee, katika jimbo la Wisconsin nchini Marekani, ambaye ameachiliwa huru kutoka kizuizini na Idara ya Uhamiaji (ICE) wiki hii, amesema kuwa amekuwa akilengwa kutokana na msimamo wake thabiti wa kutetea haki za Wapalestina.
Habari ID: 3482381   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/20

IQNA – Sauti za dua, takbira na furaha zilitawala anga ya Dearborn Heights, Michigan nchini Marekani huku mamia ya watu wakikusanyika kukata utepe wa ufunguzi wa Msikiti wa Imam Al‑Hasanain na makao makuu mapya ya Taasisi ya Kiislamu ya Amerika (IIOA).
Habari ID: 3482357   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/13

Waislamu wa China
IQNA – Kwa kutegemea mradi wa kielimu ulioendelea kwa zaidi ya miaka ishirini, Msikiti Mkuu au Msikiti wa Jamia wa Taipei katika eneo la China la Taiwan umejidhihirisha kama mfano wenye mafanikio katika kulea na kuelimisha vizazi vijavyo vya Waislamu.
Habari ID: 3482333   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/07

IQNA – Polisi wanawatafuta washukiwa baada ya msikiti mmoja katika mji wa Moncton, ulioko kusini-mashariki mwa jimbo la New Brunswick nchini Kanada, kuharibiwa kwa maandishi ya kuta (graffiti) yenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Waumini wa msikiti huo wanasema kitendo hicho ni shambulio lililolenga moja kwa moja jamii yao ya Kiislamu.
Habari ID: 3482328   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/06

IQNA – Hatua ya utawala wa Israel ya kuufunga Msikiti wa Ibrahimi katika mji wa Al-Khalil (Hebron) ni ukiukaji wa wazi wa uhuru wa kuabudu na wa haki ya wananchi wa Palestina, harakati ya muqawama ya Palestina, Hamas, imesema.
Habari ID: 3482300   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/30

IQNA – Ingawa hujuma ya kigaidi dhidi ya Msikiti wa San Diefo ilitokea umbali wa zaidi ya maili 2,000, huzuni na taharuki yake zilihisiwa moja kwa moja kote Marekani hadi kusini-mashariki mwa jimbo la Michigan siku ya Jumatano.
Habari ID: 3482267   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/22

IQNA – Watu watatu waliokuwa ndani ya Msikiti wa Kituo cha Kiislamu cha San Diego nchini Marekani wamepoteza maisha kufuatia hujuma ya kigaidi Jumatatu. Polisi wamethibitisha kuwa washambuliaji wawili, ambao ni vijana, pia wamefariki dunia, na kufanya jumla ya watu watano kupoteza maisha katika tukio ambalo maafisa wanaliita shambulizi linaloweza kuwa limechochewa na chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3482256   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/19

IQNA-Eneo la Chinga, katika mkoa wa Nambula huko kaskazini mwa Msumbiji, limeshuhudia ufunguzi wa Msikiti Mkuu wa Kati wa eneo hilo.
Habari ID: 3482181   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/30

IQNA – Sheikh Raed Salah na Sheikh Kamal al‑Khatib wamelaani marufuku ya wiki moja iliyowekwa na mamlaka za utawala haramu wa Israel kuwazuia kuingia katika Msikiti wa Al‑Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo, wakisema ni “shambulio dhidi ya dini yetu.”
Habari ID: 3482178   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/29

IQNA — Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, dua za Waislamu wa Ufilipino mjini Manila zinabeba ombi maalumu.
Habari ID: 3481996   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/26

IQNA – Kwa karne nyingi, Msikiti Mkuu wa Omari umesimama kama mlinzi kimya wa historia ya kielimu ya Gaza, hukoo Palestina huku maktaba yake ikihifadhi maandiko ya kale yaliyoandika simulizi za kupanda na kushuka kwa ustaarabu mbalimbali.
Habari ID: 3481992   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/25

IQNA – Katika mji unaojulikana kwa urithi wake wa Kikatoliki, Msikiti wa Sheikh Ibrahim Al‑Ibrahim unatoa mahali pa utulivu wa kina na ibada ya kiroho.
Habari ID: 3481989   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/25

IQNA – Kipindi maalumu cha Qur'ani kwa ajili ya kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani kinatarajiwa kutayarishwa na mwanaharakati wa vyombo vya habari wa Misri, Amr Al‑Laithi.
Habari ID: 3481944   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/16

IQNA – Katikati ya Jiji la Kuwait, mji mkuu wa nchi ya Kuwait, kuna moja ya misikiti mikubwa zaidi duniani, ambao si tu mahali pa ibada kwa maelfu ya waumini, bali pia ni jengo lenye uzito wa kiutamaduni na kielimu.
Habari ID: 3481904   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/08

IQNA- Mlipuko mkubwa umetikisa msikiti wa Waislamu wa madhehebu ya Shia katika viunga vya mji mkuu wa Pakistan wakati wa sala ya Ijumaa, na ambapo watu wasiopungua 31 wameuawa shahidi huku wengine wasiopungua 169 wakijeruhiwa. Kundi la kigaidi la ISIS au Daesh limetangaza kuhusika na hujuma hiyo.
Habari ID: 3481895   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/07

IQNA – Darasa la mafunzo ya Qur’ani linaloendelea katika Kituo cha Kiislamu cha São Paulo linatoa mfano wa vitendo wa jinsi ya kuunganisha Qur’ani, familia, elimu na jamii katika mfumo mmoja ulio thabiti ndani ya mazingira ya msikiti.
Habari ID: 3481827   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/21

IQNA – Utawala ghasibu wa Israel umetangaza mipango ya kuweka vizuizi kwa waumini Waislamu wanaotaka kufika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji mtakatifu wa al-Quds (Jerusalem0, wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3481807   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/15

IQNA – Winga chipukizi wa Klabu ya Soka ya Barcelona na Hispania, Lamine Yamal, amesema kutembelea msikiti humpa mtu utulivu wa kipekee bila kujali dini anayofuata.
Habari ID: 3481781   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/08

IQNA – Naibu mkurugenzi wa kitamaduni wa Msikiti wa Jamkaran mjini Qom, Iran, amesema zaidi ya watu 16,000 wamesajiliwa kushiriki katika ibada ya Itikafu ya mwezi wa Rajab.
Habari ID: 3481764   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/04

IQNA – Kundi la wanafunzi Waalgeria wanaoishi nje ya nchi walisoma kwa pamoja aya za Surah Al-Kahf katika Msikiti Mkuu wa Algiers.
Habari ID: 3481727   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/28