IQNA

Uturuki yaitunuku Djibouti nakala 30,000 za Qur'ani

12:01 - December 14, 2020
Habari ID: 3473456
TEHRAN (IQNA) – Shirika moja la kutoa misaada nchini Uturuki limewatunuku watu wa Djibouti nakala za Qur'ani tukufu zipatazo 30,000.

Jumuiya ya Kutoa Misaada ya Khayrat imewatunuki watu wa Djibouti nakala hizo za Qur'ani ikiwa ni katika fremu ya kampeni  ya 'Dunia Inasoma Qur'ani'.

Hivi karibun meli iliyobeba misahafu hiyo iliondoka katika mji wa bandarini wa Izmir na kuelekea Djibouti.

Ali Othman Aslanchi, mwakilishi wa Jumuiya ya Kutoa Misaada ya Khayrat mjini Izmir amesema misahafu hiyo itawafikia Waislamu wa Djibouti ambao hawana misahafu.

Ameongeza kuwa, hadi sasa wamesambaza misahafu 600,000 Uturuki na nchi zingine.

Djibouti ni nchi iliyokatika Pembe ya Afrika ambayo wakaazi wake huzungumza Kisomali huku lugha za Kifaransa  na Kiarabu na zaidi ya asilimi 94 raia milioni moja wake ni Waislamu. Wasiokuwa Waislamu aghalabu ni wazungu ambao wamechukua uraia wa nchi hiyo.

3940866

captcha