IQNA

Mwanazuoni wa Kiislamu Lebanon

Harakati za Mapambano ya Kiislamu zimepata ushindi kutokana na fikra za Imam Khomeini

19:59 - June 03, 2020
Habari ID: 3472832
TEHRAN (IQNA)- Harakati za Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) zimeweza kupata ushindi na adhama kutokana na fikra za kistratijia na kisiasa za Imam Khomeini-Mwenyezi Amrehemu- , amesema mwanazuoni wa Kiislamu nchini Lebanon.

Akizungumza na IQNA kwa mnasaba wa mwaka wa 31 tokea alipoaga duniani Imam Khomeini, Sheikh Ahmed al-Qattan, mwanazuoni mtajika wa Kisunni nchini Lebanon ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Qawluna wal Amal nchini Lebanon amesisitiza kuwa,  nchi zilizo katika mrengo wa muqawama zinaendelea kufungamana na malengo matakati ya Imam Khomeini, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu.  Amesema nchi hizo za mrengo wa muqawama sasa zinasimama kidete dhidi ya Uzayuni na uistikbari wa kimataifa.

Amesema mapamabano ya Kiislamu dhidi ya madola ya kibeberu na kiistikbari ni nukta yenye nafasi muhimu katika fikra za Imam Khomeini ambaye alifahamu kuwa njia pekee ya kukabiliana na adui ni kupitia mapambano na nguvu.

Sheikh al-Qattan pia amesema Imam Khomeini alikuwa na sifa zote ambazo kiongozi muadhamu anapaswa kuwa nazo. Aidha amemtaja Imam Khomeini kuwa mwanamageuzi ambaye aliwavutia wapenda uhuru kote duniani kutokana na fikra zake.

Mwanazuoni huyo wa Lebanon amesema Imam Khomeini alitegemea mafunzo ya Qur’ani Tukufu na Sira ya Mtume SAW kuongeza Mapinduzi ya Kiislamu hadi yalipopata ushindi.

Siku kama ya leo miaka 31 iliyopita, sawa na tarehe 14 Khordad mwaka 1368 kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Shamsia sawa na tarehe 4 Juni 1989 Milaadia, Imam Ruhullah Musawi Khomeini (MA) Muasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran aliaga dunia baada ya kuishi kwa miaka 87 katika umri uliojaa juhudi zisizo na kikomo. Kwa kutangazwa kifo cha Imam ulimwengu wa Kiislamu uligubikwa na majonzi na huzuni kubwa. Imam Khomeini (MA) alizaliwa tarehe Mosi mwezi wa Mehr mwaka 1281 Hijiria Shamsia sawa na tarehe 24 Septemba 1902 Milaadia katika mji wa Khomein ulioko katikati mwa Iran.

3902442

captcha