IQNA

Kumbukumbu ya miaka 25 iliyopita, mauaji ya kimbari ya Srebrenica

TEHRAN (IQNA) – Mauaji ya Kimbari ya Srebrenica yalijiri miaka 25 iliyopoita ambapo Waislamu zaidi ya 8000 wa mji huo waliuawa kwa umati.

Miaka 25 iliyopita katika siku kama ya jana, Waislamu zaidi ya elfu nane wa mji wa Srebrenica mashariki mwa Bosnia Herzegovina waliuawa kwa umati.

Mauaji hayo yalifanywa na Waserbia wenye misimamo mikali. Maafa hayo yalikuwa mauaji makubwa zaidi ya halaiki kuwahi kutokea barani Ulaya baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Wakati wa mauaji hayo ya kimbari, wanajeshi wa kulinda amani wa Uholanzi waliokuweko katika eneo hilo hawakuchukua hatua yoyote ya kuwahami Waislamu hao wa Srebrenica.  Jenerali Ratko Mladic, aliyekuwa kamanda wa kijeshi wa Serbia na ambaye aliongoza mauaji hayo ya Waislamu  alihukumiwa maisha jela Novemba 2017, miaka 20 baada ya mauaji hayo ya kimbari.