IQNA

Qari kutoka Iran asoma Qur'ani katika hafla ya usiku wa kuamkia mwaka mpya Bosnia

18:36 - January 02, 2026
Habari ID: 3481753
IQNA-Qari kutoka Iran ameshiriki katika usomaji Qur’an Tukufu katika hafla maalum iliyofanyika mjini Kakani, Bosnia na Herzegovina, usiku wa kuamkia Mwaka Mpya.

Kwa mujibu wa utamaduni ulioanzishwa kwa miaka kadhaa katika mji wa Kakani, Waislamu wa eneo hili hutumia usiku wa kuamkia Mwaka Mpya kujikurubisha na Qur’ani Tukufu. Sherehe ya kiroho na kitamaduni iitwayo ‘Usiku wa Qur’an’ ilifanyika Jumatano usiku kwa kuhudhuriwa na wananchi wengi, wanazuoni na familia.

Katika hafla hiyo walikuwepo pia maqari kutoka nchi kadhaa, ikiwemo  Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Zakir Effendi Ljubović, Imam wa Ijumaa wa eneo hilo, alitoa hotuba kwa hadhira, kisha akawaalika qari mbalimbali akiwemo Hadi Esfidani kutoka Iran, Hafiz Jafar Akbay kutoka Uturuki, Aziz Alili kutoka Kroatia, Hafiz Nijaz Aganhojić kutoka Bosnia na Herzegovina, na Ahmed Alili kutoka Slovenia, kusoma aya za Qur’an Tukufu.

Sehemu nyingine ya programu ilijumuisha utumbuizaji wa Tawashih (nyimbo za kidini) na Ilahiyeh (tenzi maalum za kidini zinazotolewa kwa lugha ya Kibośnia)."

3495924

 

captcha