IQNA

وَلَقَد كَتَبنا فِي الزَّبورِ مِن بَعدِ الذِّكرِ أَنَّ الأَرضَ يَرِثُها عِبادِيَ الصّالِحونَ
Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.
Suratul Anbiyaa Aya ya 105


Iwapo mwanadamu anaona  wavamizi duniani wanapora na mafasiki wanakiuka haki za wanadamu, hapaswi kudhani kuwa hii ndio hatima ya dunia, hapaswi kudhani kuwa hakuna budi na hivyo aridhie hali hii; afahamu kuwa hali hii ni ya mpito na kwamba kile ambacho ni cha dunia hii na cha maumbile ya dunia ni kuasiswa serikali adilifu na kuwa, yeye (Imamu wa Zama) atakuja.
Ayatullah Khamenei, 2005/09/20

Leo fikra ya mwanadamu iko tayari kufahamu, kujua na kuwa na yakini kuwa, mwanadamu wa hadhi ya juu atakuja na kumuokoa mwanadamu kutoka mzigo mzito wa dhulma na ukandamizaji. Hiki ni kile kile ambacho Mitume walijitahidi kuleta.  Ndicho kile ambacho Mtume wa Uislamu, kwa mujibu wa Aya ya Qur'ani, aliwaahidi wanaadamu kuwa: "…na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao…"  Surat al-A’raaf 157
Ayatullah Khamenei, 2008/11/23

Licha ya majigambo ya uistikbari na mabeberu na jitihada zao nyingi kwa mtazamo wa kifedha, kijeshi, kisiasa na kiusalama ambazo wanazitekeleza pamoja na waitifaki wao na wanofuata njia ya ubeberu katika  eneo hili (Magharibi mwa Asia) na Ulimwengi wa Kiislamu, bila shaka mustakabali mwema ni wa Uislamu.
Ayatullah Khamenei, 2015/08/17