IQNA

TEHRAN (IQNA) – Raia wa Ujerumani ambaye hivi karibuni alisilimu, alifanya sherehe yake ya harusu katika Siku Kuu ya Idd Ghadir katika Msikiti wa Nasir-ul-Mulk.

Msikiti wa Nasir-ul-Mulk, ambao pia ni maarufu kama Msikiti wa Rangi ya Waridi, ni msikiti uliojengwa nkatika zama za watawala wa Qajar na uko katika eneo la Shiraz kusini mwa Iran.

Msikiti huo umejengwa kwa usanifu majengo wenye mvuto wa Kiirani ambao ni wa aina yake.