"Diwani nzima ya Hafez imejaa mafundisho ya Qur'ani," Dk. Ali Abedi, Rais wa Chuo Kikuu cha Isfahan cha Mafunzo ya Qur'ani na Etrat, ameambia shirika la habari la IQNA.
Maoni hayo yanakuja wakati Iran inaadhimisha Oktoba 11, kama Siku ya Ktaifa ya malenga Khaja Shamsuddin Muhammad Hafidh Shirazi, ambaye ni maarufu kama Hafez
Hafiz alizaliwa mwaka 727 Hijiria Shamsia huko Shiraz moja kati ya miji ya kusini mwa Iran. Alikuwa mtaalamu wa tafsiri ya Qur'ani, falsafa na fasihi ya Kiarabu na alipata umashuhuri kwa jina la Hafidh kutokana na kuhifadhi kwake Qur'ani Tukufu kwa visomo tofauti.
Mbali na elimu hizo, Khaja Shamsuddin Muhammad Hafiz Shirazi, alikuwa mtaalamu mkubwa wa elimu ya Irfan.
Ushairi wa Hafez unachukuliwa kuwa kilele cha fasihi ya Kiajemi na bado unasomwa na kuheshimiwa sana nchini Iran na kwingineko duniani.
Mkusanyiko wake wa mashairi, unaojulikana kama Diwani ya Hafez, inapatikana katika karibu kila nyumba ya Muirani kazi yake hiyo inaendelea kuwavutia wasomaji kutokanana maarifa yake ya kina na lugha nzuri.
"Mbali na kuwa mhifadhi wa Qur'ani Tukufu, Hafez pia alikuwa akifundisha Tafsisi ya Qur'ani ya Al-Kashshaaf iliyoandikwa na Zamakhshari, ambayo ni tafsiri ya Qur'ani iliyotukuka kutokana na ufasaha," aliongeza Abedi.
"Kama mshairi na gwiji wa ufasaha wa kuzungumza na muziki, Hafez alikuwa na mtindo wa kipekee katika mtazamo wake wa Qur'ani Tukufu," alisema msomi huyo.
Unaweza kutambua maana ya aya za Qur'ani Tukufu kupitia ushairi wa Hafez, alisema, akinukuu beti la Hafez lisemalo : "Kati ya Huffadh wote za ulimwengu, hakuna hata mmoja aliyekusanya siri za hekima na nukta za Qur'ani kama nilivyokusanya."
"Hafez pia anasema mahali pengine kwamba ushairi wake ni 'kilele cha elimu' na elimu hii ni nini? Ni mafundisho safi ya Quran," Abedi aliongeza.
Kwa mfano, tafakari hapa wakati Hafez anavyoakisi fikra ya Qur'ani kwa kusema: 'Shetani huwakimbia wale wanaosoma Qur'ani.' Maana yake ni kwamba mashetani hawakaribii wale wanaosoma Qur'anI, kwani wao ni watu wa nuru, na Qur'anI yenyewe ni nyepesi, kama asemavyo Mwenyezi Mungu: Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha.' (Surah Maidah, aya ya 15), aliongeza mwanachuoni huyo.
4241731