IQNA

Iran yajibu tuhuma zisizo na msingi za utawala wa Saudia

11:21 - September 30, 2020
Habari ID: 3473217
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nchi za Nje ya Iran amejibu madai ya uongo yaliyotolewa na Saudi Arabia ikisema kuwa imenasa kundi la magaidi lenye mfungamano na Iran na kusema: Watawala wa Saudia wanapaswa kuchagua njia ya ukweli hekima na busara badala ya kueneza uzusha na imlaa wanazopewa na madola mengine.

Saeed Khatibzadeh amesema kuwa tuhuma hizo za Saudi Arabia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ni mwendelezo wa misimamo ya kukaririwa na isiyo na msingi ya Wasaudia katika miaka ya karibuni. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, watawala wa Riyadh wameweka kando mantiki ya kisiasa na mara hii katika kalibu na fremu ya maonyesho ya darala la tatu, wanatumia propaganda chafu dhidi ya Iran kama wenzo wa kupotosha fikra za walimwengu na kuficha sera na siasa zao zilizofeli.

Khatbzadeh ameongeza kuwa, tuhuma zisizo na msingi na za kukaririwa wa watawala wa Saudi Arabia hazitaifikisha Saudia katika malengo yake. 

Matamshi hayo yametolewa baada ya msemaji wa serikali ya Saudia kudai kwamba nchi hiyo imekamata watu 10 waliokuwa na silaha na kwamba watatu miongoni mwao wamepewa mafunzo na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran.

3926193

Kishikizo: saudi arabia iran
captcha