IQNA

Kumbukumbu ya Ayatullah Taskhiri, mbeba bendera ya umoja wa Kiislamu + Video

TEHRAN (IQNA)- Ayatullah Mohammad Ali Taskhiri (1944-2020) anatajwa kama mmoja kati ya maulamaa mashuhuri zaidi duniani waliokuwa mstari wa mbele kutetea umoja wa Kiislamu.

Alizaliwa katika familia ya Kiirani huko Najaf, Iraq mnamo Oktoba 14, 1944. Alisoma Uislamu katika mji huo lakini baadaya alitimuliwa na utawala wa Kibaath wa Iraq kutokana na harakati zake za kisiasa. Aliporejea Iran, Taskhiri alianza kufunza katika chuo cha kidini au Hauza katika mji wa Isfahan.

Mwaka 1981 aliteuliwa kuwa naibu mkuu wa masuala ya kimataifa katika Shirika la Maendeleo ya Kiislamu nchini Iran na mwaka 2001 Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alimteua kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Umoja wa Kiislamu. Alibakia katika nafasi hiyo kwa muda wa miaka 12 ambapo alitoa huduma kubwa katika harakati za kukurubisha madhehebu ya Kiislamu. Ayatullah Taskhiri aliaga dunia Agosti 14, 2020 kutokana na matatizo ya moyo.

4006180