IQNA

Msikiti wa miaka 1300 wagunduliwa Iraq

12:14 - November 27, 2021
Habari ID: 3474607
TEHRAN (IQNA) – Msikiti wa matope uliojengwa katika zama za utawala wa Bani Ummaya umegunduliwa nchini Iraq.

Wataalamu wa Iraq wakishirikiana na wataalamu wa Jumba la Makumbusho la Uingereza wamegundua msikiti huo ambao unaaminika kujengwa mwaka 60 Hijria au 679 Miladia katika jimbo la Dhi Qar kusini mwa Iraq.

Msikiti huo umegunduliwa katika mji wa Al Rafa’i na una upana wa mita nane kwa tano na uko kati kati ya eneo la makazi.

Ali Shalgham, mkuu wa utafiti katika jimbo hilo amesema kugunduliwa msikiti huo ni hatua muhimu kwani ulijengwa kwa matope katika zama za awali za Uislamu.  Amesema ni maeneo machahce sana ya zama za Bani Umayya yaliyogunduliwa kwani majengo mengi ya wakati huo yameshatoweka.

Jimbo la Dhi Qar lina idadi kubwa ya mabaki ya kale ikiwemo miji ya kale za Mesopotamia katika eneo la Ur.

Katika muda wa miaka 20 wa vita na machafuko Iraq, kumeshuhudiwa wizi mkubwa wa turathi za kale za nchi hiyo katika kile kinachoonekana ni jama za makusudi za kufuta ustaarabu wa nchi hii ya Kiarabu na Kiislamu.

3476669

captcha