IQNA

Kikao cha Kujikurubisha na Qur’ani katika Siku ya Kwanza ya Ramadhani

Sambamba na siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kumefanyika 'Mahafali ya Kushikamana na Kujikurubisha na Qur’ani.' Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Husainiya ya Imam Khomeini jijini Tehran mnamo Machi 2, 2025 na kuhudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei.