Video ya wimbo wa ‘Lazima Tuinuke’ yatolewa kwa Kiingereza
IQNA – Video ya wimbo wa kishujaa wenye jina la “We Must Rise” (Lazima Tuinuke) imetolewa rasmi kwa lugha ya Kiingereza ambapo muimbaji ni Mahdi Dardashtian. Wimbo huu ni kazi iliyosikika kwa sauti za huzuni katika majilisi za maombolezo katika majimbo mbalimbali nchini Marekani wakati wa usiku wa mwezi mtukufu wa Muharram.
Kazi hii imedhihirisha mshikamano wa kina wa nyoyo za watu kutoka mataifa tofauti; watu waliojitokeza kuomboleza msiba wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuonyesha mshikamano wa dhati na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hili ni dhihirisho tosha kuwa huzuni hii haijafungwa na mipaka ya kijiografia, bali inagusa nyoyo za watu huru ulimwenguni kote, ikionyesha kuwa mapenzi kwa shakhsia wa haki hayajui mipaka.
copied
https://iqna.ir/H0EbwQ