IQNA

RIPOTI

Saudia ilitumia mamluki wa Ufaransa kuwahujumu Waislamu Makka mwaka 1979

17:22 - February 04, 2020
Habari ID: 3472438
TEHRAN (IQNA)- Ripoti mpya imefichua kuwa, Saudia Arabia ilitumia mamluki wa Ufaransa kuua na kukandamiza Waislamu waliokuwa wameanzisha mwamko dhidi ya ufalme wa Saudi Arabia katika Msikiti Mtakatifu wa Makka (Al-Masjid Al-Haram) mwaka 1979.

Askari wa Saudia  Juhayman al-Otaibi na kundi lake walianzisha mgomo na wakachukua udhibiti wa Al Ka'aba mnamo Novemba 20,1979 katika siku ya kwanza ya Mwezi wa Muharram 1400 ambapo walisisitiza kuwa kitendo chao kilikuwa njia ya utawala wa ukoo wa Aal Saud ambao walisema ulikuwa umepoteza uhalali wake kutokana na ufisadi wkae mkubwa wa kifedha na kimaadili na kuiga madola ya Magharibi. Wafalme wa Saudi Arabia kwa kawaida hujinadi kuwa ni wahudumu wa Haram Mbili Takatifu za Kiislamu za Makka na Madina.

Tukio hilo liliendelea kwa muda wa wiki mbili kabla ya 'kikosi maalumu cha askari wa Saudia' kuingia katika msikiti huo na kusambaratisha mzingiro mzingor wa wanamgambo hao.

Ripoti mpya iliyosambazwa Jumatatu na Televisheni ya Al Jazeera yenye makao yake Doha, Qatar imesema madola ya kigeni yalihusika katika oparesheni hiyo Disemba 1979 ya kukandamiza mwamko huo wa Waislamu katika Msikiti Mtakatifu wa Makka. Ripoti hiyo inaenda kinyume na madai ya utawala wa Saudia kuwa ni askari wa Saudia pekee waliohusika katika oparesheni hiyo.

Al Jazeera imesema Saudi Arabia iliomba msaada kutoka  Ufaransa na Marekani  ambapo mamluki wasiokuwa Waislamu wa nchi hizo waliingia katika Al-Masjid Al-Haram na kukandamiza mwamko huo. 

Ripoti hiyo imedokeza kuwa waziri wa mambo ya ndani wa Saudia wakati huo alikutana na kamanda wa Kikosi Maalumu cha Ufaransa Paul Barrell.

"Barell aliitaka nchi yake itume mabomu elfu mbili ya gesi, yenye uzito wa tani saba, mabomu ambayo yalikuwa na uwezo wa kumpofua jicho mlengwa," imesema ripoti hiyo.

Kinyume na walivyodai Wasaudi kuwa oparesheni hiyo ilipelekea watu 300 kupoteza maisha, wakiwemo 26 waliokuwa katika ziara ya Umrah, Barell anasema oparesheni hiyo ilipelekea kuuawa watu 5,000 wakiwemo watu 3,000 waliokuwa katika ibada ya Umrah.

Kiongozi wa mwamko huo, Al Otaibi, alinyongwa hadahrani mjini Makka Januari 9, 1980 na wenzake w63 nao pia walinyongwa katika miezi iliyofuata.

3470528

captcha