IQNA

Msikiti wa Kihistoria mjini Durban, Afrika Kusini wateketea moto

14:12 - August 26, 2020
Habari ID: 3473104
TEHRAN (IQNA) – Msikiti wa kihistoria uliojengwa miaka 139 iliyopita umeteketea moto katika mji wa Durban, Afrika Kusini.

Inaaminika kuwa hitilafu ya umeme ndio chanzo cha moto huo uliotokea Jumatatu katika msikiti huo unaojulikana kama Grey Street Mosque.

Faisal Suliman, mwenyekiti wa Mtandao wa Waislamu Afrika Kusini amesema moto huo unaaminika kuanza katika moja kati ya nyumba zilizojuu ya msikiti huo. Amesisitiza kuwa moto uwezekano mkubwa ni kuwa moto huo haukuanza kwa makusudi.

Wazimamoto walifanikiwa kuzima moto huo baada ya masaa mawili. Waislamu wamesikitishwa na tukio la kuteketea moto msikiti huo wa kihistoria wenye uwezo wa kuwabeba waumini 7,000.

Msikiti huo ambao ni kati ya majengo ya aina yake kati mwa Durban umewahi kutembelewa na watu mashuhuri kama vile Shujaa Nelson Mandela, muimbaji mashuhuri wa Uingereza Yusuf Islam ambaye kabla ya kusilimi alijulikana kama Cat Stevens na bingwa wa masumbwi Muhammad Ali.

3918894

captcha