IQNA

Waislamu Afrika Kusini walaani marufuku ya adhana

20:47 - September 08, 2020
Habari ID: 3473149
TEHRAN (IQNA) – Waislamu wa mjini Durban Afrika Kusini wamelaani hatua ya mahakama moja nchini humo kuamuru adhana ipigwe marufuku katika msikiti mmoja mjini humo.

Mawakili wa Madrassah ya Isipingo Beach, ambayo imetakiwa isiadhini kwa vipaza sauti kufuatia malalamiko ya jirani, wanakusudia kukata rufaa kufuatia hukumu hiyo.

Mwezi uliopita, jaji Sidwell Mngadi wa Mahakama Kuu ya Durban alitoa hukumu ya kupiga marufuku adhana kufuata ombo la Chandra Giri Ellaurie ambaye ni maarufu kwa msimmamo wake wa chuki dhidi ya Uislamu.  Ellaurie amedai kuwa adhana inaupa mtaa huo utambulisho wa kipekee wa Kiisamu jambo ambalo analipinga.

Jaji huyo aliamuru Madrasah Taleemudeen Islamic Institute kuhakikisha kuwa adhana haisikiki katika nyumba ya Ellaurie, ambayo iko milango miwili tu kutoka madrassah hiyo.

Mawakili wa madrasah hiyo wamekata rufaa na kusema jajai mnagadi alikosea kwa sababu kadhaa na hivyo kesi hiyo inapaswa kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Rufaa kwa maslahi ya haki na ummah.

Aidha wamesema jaji huyo hakuzingatia haki ya dini kwa kumpa haki zaidi mlalamishi badala ya haki ya kuabudu katika madrasah, wanafunzi na wanaoswali hapo.

3921558

captcha