IQNA

Al Hakim asisitiza Iraq haitauruhusu ugaidi urejee tena nchini humo

11:21 - February 14, 2021
Habari ID: 3473648
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Hekima ya Kitaifa ya Iraq haitauruhusu urudi tena nchini humo.

Sayyid Ammar al Hakim ametoa sisitizo hilo Ijumaa katika hauli na kumbukumbu ya siku aliyouawa shahidi Ayatullah Sayyid Muhammad Baqir al Hakim iliyofanyika katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad na akaongeza kwamba: “ ili kulinda usalama wa nchi kuna ulazima wa kuwa macho na kufanya jitihada za kiintelijensia na za uchukuaji hatua za tahadhari; na kwamba serikali nayo inapaswa kutekeleza mpango uliopitishwa na bunge kuhusiana na askari wa Marekani kuondoka nchini Iraq.”

Kiongozi wa Harakati ya Hekima ya Kitaifa amesema, ana matumaini serikali mpya ya Marekani itabadilisha muelekeo kuhusiana na masuala ya eneo; na akasisitiza kuwa kurejea haraka nchi hiyo katika makubaliano ya nyuklia na kuondoa haraka vikwazo ilivyoliwekea taifa la Iran ni mambo ya lazima kwa ajili ya kurejea amani na uthabiti katika eneo hili.

Sayyid Ammar al Hakim amekumbusha pia kuwa, Palestina ndilo suala kuu na la msingi kwa nchi za Kiislamu na Kiarabu na kwamba uungaji mkono usio na mpaka wala kikomo wa haki za kiuadilifu za taifa la Palestina utaendelea.

Kiongozi wa Harakati ya Hekima ya Kitaifa ameeleza kwamba, shahidi Al Hakim aliuawa shahidi kwa kupigania uhuru wa taifa lake na kubadilisha mlingano wa kidikteta uliokuwepo; na leo hii pia wananchi wa Iraq wako katika kipindi ambacho hatari na ugumu wake hautafautiani na wa kipindi cha huko nyuma.

3473961

captcha