IQNA

Ugaidi wa Marekani

Marekani yalaaniwa kwa kumuua kigaidi mwanamapambano wa Iraq

18:57 - February 09, 2024
Habari ID: 3478325
IQNA-Utawala wa Marekani unaendelea kulaaniwa kufuatia hujuma yake ya kigaidi iliyopelekea kuuawa shahidi Abu Baqer al-Saadi, mmoja wa makamanda wa muqawama wa Kiislamu nchini Iraq.

IQNA-Utawala wa Marekani unaendelea kulaaniwa kufuatia hujuma yake ya kigaidi iliyopelekea kuuawa shahidi Abu Baqer al-Saadi, mmoja wa makamanda wa muqawama wa Kiislamu nchini Iraq.

Kwa kutoa taarifa, harakati ya Nujaba ya Iraq imelaani vikali hujuma hiyo ya kigaidi ya Marekani katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad dhidiya kamanda huyo.

Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) ilisema Jumatano kwamba vikosi vyake vilifanya mashambulizi ya anga mjini Baghdad, na kumuua kamanda mkuu wa harakati ya muqawama ya Kataib Hizbullah ya Iraq akiwa ndani ya gari.

Ugaidi huo umelaaniwa vikali na Harakati ya Nujaba ya Iraq ambayo imesema: Kamanda al-Saadi alikuwa mwanachama wa kikosi rasmi kinachofungamana na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iraq. Uko wapi uhuru wa Iraq, utakatifu wa damu na mamlaka ya kujitawala?

Nayo Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na ile ya Jihadul Islami zimetoa taarifa tofauti na kulaani shambulizi la Marekani dhidi ya wanamapambano wa Iraq, mashariki mwa mji mkuu, Baghdad.

Katika taarifa yake, HAMAS imesema, tunalaani shamblio la kinyama la Jumatano usiku lililofanywa na Marekani mjini Baghdad ambalo limeua viongozi wa muqawama wa nchi hiyo. Shambulio hilo ni uvunjaji wa wazi wa haki ya kujitawala na usalama wa Iraq na ni muendelezo wa kutumikia njama za utawala dhalimu wa Israel. 

HAMAS imetoa mkono wa pole kwa serikali na wananchi wa Iraq na kusema kuwa serikali ya Joe Biden huko Marekani ndiyo inayobeba dhima ya matokeo yoyote mabaya yatakayotokea kwenye eneo hili. 

Kwa upande wake, Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina imesema kwenye taarifa yake kwamba inalaani vikali shambulio la Marekani nchini Iraq ambalo limepelekea kuuawa shahidi viongozi wa kambi ya muqawama nchini humo.

Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen nayo imesema kuwa, mashambulizi ya mara kwa mara ya Marekani dhidi ya wananchi wa Iraq hayawezi kuteteresha msimamo wao imara wa kuliunga mkono taifa la Palestina. 

Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa muqawama wa Iraq na wengine kadhaa waliuawa shahidi katika shambulio la jana usiku la Marekani nchini Iraq.

Wananchi wa Iraq wamefanya maandamano hadi kwenye eneo lilipofanyika shambulizi hilo, ili kulaani jinai hizo za dola vamizi la Marekani nchini mwao na wamezidi kutilia mkazo wajibu wa kutimuliwa haraka wanajeshi wa Marekani nchini Iraq.

4198732

captcha