IQNA – Saa chache tu baada ya ushindi wa Abdul El-Sayed katika uchaguzi wa awali wa Seneti wa chama cha Democratic huko Michigan, matusi na chuki mtandaoni dhidi yake viliongezeka kwa kasi kubwa, kulingana na utafiti mpya wa Kituo cha Utafiti wa Chuki Iliyopangwa (CSOH).
Habari ID: 3482626 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/15
IQNA – Akilaani vitendo vya mara kwa mara vya kuidhalilisha na kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu kama vitendo vya “Kizayuni na Kimarekani,” kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, Sayyid Abdul-Malik Badruddin al-Houthi, amesema vitendo hivyo vya kukufuru na kukiuka heshima ya Qur’ani ni sehemu ya uadui mpana zaidi dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3482622 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/14
IQNA – Katika kitovu cha eneo la Mississippi Delta, mwanamke Mwislamu amekalia kiti cha mahakama ya manispaa akiwa na jina la kihistoria na wimbi la barua za chuki.
Habari ID: 3482615 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/11
IQNA – Moto ulikuwa haujazimika vyema katika Jumuiya ya Kiislamu ya Al-Aqsa, iliyoko kaskazini-mashariki mwa Philadelphia, Marekani mwezi uliopita, wakati wachunguzi wa shirikisho walipoungana kimyakimya na wazima moto wa eneo hilo katika eneo hilo la tukio lililoathiriwa na moto.
Habari ID: 3482596 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/08
IQNA – Vyombo vya habari vya Israel vimeonyesha wasiwasi kufuatia ushindi wa daktari Mmisri-Mmarekani, Abdul El-Sayed, katika kura za mchujo za Chama cha Democratic kwa kiti cha Seneti ya Marekani katika jimbo la Michigan, vikilitaja tukio hilo kuwa pigo muhimu kwa makundi yanayounga mkono Israel nchini Marekani.
Habari ID: 3482593 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/07
IQNA – Baraza la Jiji la McKinney, jimboni Texas nchini Marekani, limeidhinisha kwa kauli moja mpango wa kujengwa kwa msikiti mpya uliopendekezwa na Jumuiya ya Kiislamu ya McKinney, licha ya wasiwasi uliotolewa na baadhi ya wakazi kuhusu athari zinazoweza kujitokeza kwa jamii inayozunguka eneo hilo. Uamuzi huo wa kura 7-0 ulifuatia kikao kirefu na wakati mwingine chenye mvutano, ambapo takriban wakazi 150 walizungumza, baadhi wakiunga mkono na wengine wakipinga mradi huo.
Habari ID: 3482592 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/07
Mtazamo
IQNA – Mchambuzi wa kisiasa kutoka Lebanon anaamini kuwa mvutano unaoendelea katika Lango Bahari La Hormuz si mapambano ya kawaida juu ya njia ya majini, bali ni vita vikali vya kuamua hatima na utambulisho wa mfumo wa kiusalama katika eneo la Asia Magharibi.
Habari ID: 3482543 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/27
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ameisifu harakati ya Hizbullah kwa msimamo wake thabiti na usioyumba katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema, kuwa uimara wa harakati hiyo ya Lebanon ni ujumbe wenye nguvu wa ukombozi kwa mataifa yaliyodhulumiwa duniani kote.
Habari ID: 3482542 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/27
IQNA – Muungano wa Walimu wa Marekani (American Federation of Teachers - AFT) umeitupia lawama utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kusababisha mgogoro wa walimu katika ardhi za Palestina, huku ukitoa wito wa kukomeshwa kwa uchokozi dhidi ya Lebanon na kuondolewa kwa mzingiro haramu uliowekwa kwenye bandari za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3482520 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/21
IQNA – Mfanyakazi mmoja Mwislamu wa vibanda vya biashara amechomwa kisu zaidi ya mara 15 ndani ya kituo cha ununuzi (mall) huko Utah, Marekani, na mtu ambaye baadaye alikiri kwa polisi kuwa alikusudia kumuua “kwa sababu ya dini yake.”
Habari ID: 3482498 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/17
IQNA-Iran imeonya kwamba italenga kila miundombinu iliyosalia katika eneo hili iwapo miundombinu yake itashambuliwa.
Habari ID: 3482494 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/16
IQNA – Vatikani (Vatican) imekataa jaribio la balozi wa utawala wa Trump katika Vatikan la kuwasilisha ukosoaji wa Papa Leo wa XIV dhidi ya vita vya Marekani dhidi ya Iran kana kwamba ulikuwa uingiliaji wa kisiasa badala ya msimamo wa kidini.
Habari ID: 3482484 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/14
IQNA-Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo asubuhi vimetekeleza operesheni ya pamoja ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani nchini Jordan, Kuwait, Qatar, Oman na Bahrain, ikiwa ni hatua ya kujibu mashambulizi endelevu ya Marekani dhidi ya maeneo ya kusini mwa Iran.
Habari ID: 3482473 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/12
IQNA-Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza rasmi kuwa, katika hatua ya kwanza ya kujibu uchokozi wa Marekani wa usiku wa kuamkia leo, vikosi vya wanamaji na anga vya Jeshi hilo, katika operesheni ya pamoja ya makombora na ndege zisizo na rubani (drones), vimetekeleza kwa mafanikio mashambulizi makali dhidi ya shabaha 85 muhimu vya kijeshi la Marekani na kutungua ndege moja ya kisasa ya kijasusi ya adui aina ya MQ9.
Habari ID: 3482458 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/08
IQNA-Wakati shughuli za mazishi na kuaga mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, zikiendelea nchini Iran, Waislamu na wafuasi wake nchini Marekani wameungana kufanya ibada za maombolezo kufuatia kuondoka kwa kiongozi huyo.
Habari ID: 3482449 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/06
IQNA-Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa limeendesha oparesheni kubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani (droni) dhidi ya vituo nane vya kijeshi vya Marekani katika kanda hii, likiitaja hatua hiyo kuwa “jibu madhubuti” dhidi ya uchokozi mpya wa Marekani kwenye ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3482414 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/28
IQNA-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Mkataba wa Maelewano (MoU) wa kumaliza vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran haukuwa matokeo ya shinikizo au kulazimishwa, bali ni zao la ustahimilivu na nguvu ya taifa shupavu la Iran.
Habari ID: 3482399 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/24
IQNA-Rais wa Iran ametoa wito wa ushirikiano wa karibu zaidi miongoni mwa nchi za Kiislamu, akisema Iran imenyoosha “mkono wa urafiki” kwa nchi za kanda hii katika harakati za kutafuta mfumo mpya wa usalama.
Habari ID: 3482398 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/24
IQNA – Mwigizaji maarufu wa Hollywood, Giancarlo Esposito, amethibitisha kuingia kwake katika dini ya Kiislamu baada ya kutamka Shahada, nguzo kuu ya imani ya Kiislamu, na kushiriki katika ibada ya swala msikitini pamoja na wahudumu wenzake wa uzalishaji wa filamu.
Habari ID: 3482393 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/23
IQNA – Rais wa msikiti mmoja mjini Milwaukee, katika jimbo la Wisconsin nchini Marekani, ambaye ameachiliwa huru kutoka kizuizini na Idara ya Uhamiaji (ICE) wiki hii, amesema kuwa amekuwa akilengwa kutokana na msimamo wake thabiti wa kutetea haki za Wapalestina.
Habari ID: 3482381 Tarehe ya kuchapishwa : 2026/06/20