IQNA

Video: Watoto wa Malawi wakisoma Qur'ani pamoja

IQNA – Katika mandhari ya vijijini vya Malawi, taswira za watoto wakishiriki kwa ari katika miduara ya kisomo cha Qur'ani Tukufu zimeanza kuvutia mitandaoni, zikidhihirisha mchango hai wa jamii ya Waislamu wachache nchini humo.

Katika mitandao ya kijamii ya Kiarabu, video zilizosambazwa hivi karibuni zinaonesha watoto wa Malawi wakikusanyika nje, wakisoma na kuhifadhi aya za Qur'an kwa ari kubwa, licha ya hali ngumu za maisha. Mandhari ya tukio inaonekana kuwa ya mbali, yenye mandaki ya jangwa, kusini mwa Malawi.

Malawi ni nchi iliyoko kusini mashariki mwa Afrika, yenye idadi ya watu takriban milioni 21. Ukristo ndio dini kuu nchini humo. Sensa ya mwaka 2018 ilibainisha kuwa Waislamu ni takriban asilimia 13.8 ya wakazi wote. Sehemu kubwa ya Waislamu hao ni wa madhehebu ya Sunni, na wengi wao wanaishi karibu na mwisho wa kusini wa Ziwa Malawi.

4315068

Kishikizo: malawi ، qurani tukufu