"Ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu ni jambo ambalo limepelekea Waislamu wabaguliwe. Tunatengwa kwa njia nyingi sana. Aidha wengi hawatufahmu katika taasisi nyingi," amesema Sheikh Jafalie Kwawings, Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Waislamu kwa Ajili ya Demokrasia na Maendelea (MUSFORD), taasisi ambayo imeanzisha mpango huo.
"Sisi kawaida huwa watu wa mwisho kukumbukwa katika masuala ya maendeleo nchini. Hii ni ishara ya wazi ya namna Waislamu wanavyochukiwa katika nchi hii. Kwa kushirikiana na vyombo vya habari, tutaweza kutoa mafunzo kwa waandishi habari kuhusu masuala kadhaa kuhusu Uislamu ili kuelimisha umma wa nchi," ameongeza.
Sheikh Kawinga amevilaumu vyombo vya habari kwa kuchochea zaidi chuki dhidi ya Waislamu nchini humo.
Malawi ina idhaa moja ya Waislamu ijulikanayo kama Radio Islam lakini haina uwezo wa kutosha wa kuzuia ubaguzi dhidi ya Waislamu.
Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa Malawi baada ya Ukristo ambapo Waislamu ni asilimia 36 ya wakaazi wote milioni 15 katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika...mh