IQNA

Waislamu, Wakristo Malawi wapongeza ujenzi wa msikiti mpya

9:43 - March 20, 2022
Habari ID: 3475055
TEHRAN (IQNA)- Msikiti mpya uliopewa jina la Taqwa umefunguliwa katika mji wa kibiashara wa Malawi, Blantyre.

Msikiti huo uko katika eneo la Ginnery Corner karibu na Hospitali Kuu ya Queen Elizabeth na umaridadi wake umewavutia Waislamu wengi na Wakristo wa eneo hilo.
“Nilipita karibu na msikiti huo wakati wa jioni na niliona mandhari yenye mvuto,” amesema mtumizi wa Twitter nchini Malawi.
Mtumizi mwingine Mkristo wa Twitter alisema baada ya kuona umaridadi huo, amefahamu ni kwa nini msikiti huo ulichukua miaka minne kuujenga.
Waislamu kutoka maeneo mengine Malawi wanasema kila wanapotembelea Blantyre watafika katika msikiti huo kuswali na pia kuona umaridadi wake. Waumini wa Kiislamu nchini Malawi wamemuomba Mwenyezi Mungu awape ujira mwema wale wote waliohusika katika ujenzi wa
3478238

Kishikizo: malawi
captcha