Mpango huo ulianzishwa na Al Haj Kawinga baada ya machafuko ya hivi karibuni kusini mwa Malawi katika wilaya ya Blantyre wakati baadhi ya wanakijiji walizozana na Waislamu kuhusu kipande cha ardhi ambacho kinamilikiwa na Jumuiya ya Kiislamu katika eneo la Chadzunga.
Kufuatia machafuko hayo, polisi waliwatia mbaroni makumi ya Waislamu huku wakiwapachika jina la “Boko Haram” na hivyo kuibua hisia dhidi ya Waislamu katika nchi hiyo tulivu.
Waislamu nchini Malawi walilaani vikali kitendo hicho cha polisi na hivyo wakaamua kutoa mafunzo kwa umma kuhusu Uislamu.
Katibu Mkuu wa Tume ya Kiislamu ya Amani na Uhuru Hassan Chimwala amesema iwapo hakutakuwepo azma ya wafuasi wa dini mbali mbali kuheshimiana basi yamkini Malawi ikatumbukia katika vita vya kidini. Ametoa wito kwa Waislamu kushikamana na kuungana kwa ajili ya nchi yao.../mh