IQNA

Waungaji mkono Wapalestina wanaodhulumiwa

Waislamu Malawi walaani jinai za Israel dhidi ya Palestina (+Video)

18:49 - November 02, 2023
Habari ID: 3477831
LILONGWE (IQNA) - Kundi la Waislamu, wakiwemo wanafunzi chuo cha Kiislamu, walifanya maandamano nchini Malawi mauaji ya kimbari yanayotekelezwa wa utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza.

Kituo cha Kiislamu cha Malawi kiliandaa mjumuiko huo, ambao ulihudhuriwa na wanafunzi wa tawi la Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa nchini humo.

Wanafunzi hao walibeba mabango  na kutoa nara za kulaani jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel hasa mauaji ya watoto huko Palestina.

Malawi ni nchi isiyo na bandari kusini mashariki mwa Afrika. Takriban asilimia 25 ya wakazi nchini humo ni Waislamu ambao aghalabu wanaishi katika Kanda ya Kusini.

Utawala wa haramu wa Israel umekuwa ukiushambulia Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya wiki tatu, baada ya operesheni ya kushtukiza iliyoanzishwa na Hamas kwa lengo la kujibu jinai za utawala huo katili.

Mashambulizi hayo ya Israel hadi sasa yamepelekea takriban Wapalestina 9,000 kupoteza maisha tokea Oktoba 7 ambapo  wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.

3485853

Habari zinazohusiana
captcha