Tovuti ya Yemen Times imeripoti kuwa, Kamati ya Utamaduni, Vyombo vya Habari na Utalii ya Bunge la Yemen imetaka kufanyike uchunguzi katika idara ya utalii, athari za kale majumba ya makumbusho ya Wizara ya Utamaduni baada ya kuibiwa nakala za kale za Qur’ani na panga za zamani kutoka kwenye Jumba la Makumbusho la Taifa.
Mkuu wa Idara ya Utalii na Turathi za Kale ya Yemen Abduh al Hudhaifi amesema kuwa kuibwa kwa athari za kale za Yemen ni sawa na kuibwa utambulisho na historia ya taifa la nchi hiyo.
Ameongeza kuwa nakala za Qur’ani zilizoibwa katika Jumba la Makumbusho la Taifa ni nadra sana na moja na nakala hizo iliandikwa miaka 1300 iliyopita. Vitabu vya historia vinasema kuwa wahyi na ufunuo ulikamilika kuteremshwa kwa Nabii Muhammad (saw) miaka 1381 iliyopita.
Hudhaifi amesema kuwa Bunge la Yemen pia limeunda kamati maalumu itakayofanya uchunguzi wa kuwakamata waliohusika na wizi wa nakala hizo za Qur’ani na kwamba Rais Abduh Mansour wa Yemen pia ameanzisha uchunguzi maalumu wa kufuatilia suala hilo. 1310032