Kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Palestina, msafara huo unapangiwa kukutana na kundi jingine la meli na boti zilizoondoka katika bandari za Uturuki na Ugiriki ili kuunganisha msafara huo kabla ya kuelekea katika kituo chake cha mwisho.
Wasemaji wa msafara huo walisema kuwa meli zinaendelea na safari yao kulingana na ratiba ya “Spring 2026 Mission”, licha ya kuwepo kwa shinikizo kubwa la kisiasa na kisheria kutoka kwa baadhi ya pande za kimataifa zinazojaribu kuzuia safari hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, meli za msafara huo ambazo zimebeba wanaharakati kutoka nchi 39 zinaendelea na safari yao, na iwapo hazitazuiliwa baharini, zinatarajiwa kufika katika maji ya Palestina katika siku zijazo.
Mwezi Septemba uliopita, msafara huo uliondoka kutoka Hispania, na hatimaye ulijumuisha boti 43 pamoja na watu 462.
Kabla haujafika Gaza, vikosi katili vya vya Israel vilivamia meli hizo na kuwakamata washiriki waliokuwamo, akiwemo mwanaharakati wa mazingira kutoka Sweden, Greta Thunberg.
3497278