
Askofu William Shomali, naibu wa Patriarka wa Kanisa Katoliki la Kilatini katika al-Quds (Jerusalem) amesema kuwa alitazama video ya tukio hilo la kusikitisha na kulitaja kuwa “lenye uchungu, la kutisha, na zito sana.”
Ameongeza kuwa: “Mtawa huyo hivi sasa ni dhaifu kiafya. Mshambuliaji alimsukuma kwa nguvu kutoka nyuma, na kumsababisha aanguke chini baada ya kichwa chake kugonga jiwe lililoinuka. Kisha alirudi na kumkanyaga kabla ya kuzuiwa”
Askofu Shomali pia amesisitiza “hitaji la kutoa elimu kwa wale wenye itikadi za kibaguzi.”
Ameongeza: “Mshambuliaji kurudi tena na kumpiga teke baada ya kumuumiza tayari kunafanya kitendo hiki kuwa cha ukatili mkubwa zaidi.”
Kuhusu kukamatwa kwa mshambuliaji huyo wa Kizayuni amesema polisi wa utawala wa Israel “hawajakuwa wakichukua hatua za haraka katika matukio mengine kama haya.”
Aidha Askofu Mkuu Ataullah Hanna, ambaye ni mkuu wa Othodoksi ya Kigiriki katika mji wa al-Quds (Jerusalem), ameonya kuwa matukio ya aina hii “yanaakisi wasiwasi unaoongezeka kuhusu mustakabali wa uwepo wa Kikristo katika Ardhi Takatifu inayokaliwa kwa mabavu.”
Katika ujumbe wa mitandao ya kijamii, Askofu Hanna amesema kuwa “shambulio dhidi ya mtawa katika mji wa al-Quds linakuja katikati ya ukiukaji unaozidi dhidi ya taasisi za Kikristo mjini humo.”
Katika ujumbe huo, alionya kuwa mashambulizi kama haya “hayako tena katika sura ya matukio ya hapa na pale, bali ni muendelezo unaotishia uwepo wa Kikristo.”
Ameitaka pia jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kukomesha ukatili huo.
Miaka ya karibuni imekuwa na ongezeko dhahiri la mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya viongozi wa Kiislamu na Kikristo na dhidi ya maeneo matakatifu katika eneo la al-Quds Mashariki.
Shambulio hili linakuja baada ya video iliyosambaa mwezi uliopita, ikimuonyesha askari wa jeshi katili la Israel akibomoa Sanamu ya Nabii Isa ambayo ni nembo ya Ukristo kwa nyundo kubwa, tukio ambalo limelaaniwa dunaini kote.
Viongozi wa Kanisa wamekuwa wakitoa wito mara kwa mara kwa mamlaka za Israeli kuchukua hatua thabiti kukomesha mashambulizi kama haya. Hatahivyo wakuu wa Israel hawachukua hatua jambo ambalo limepelekea matukio kama hayo kuongezeka.
4349666