IQNA

Qari wa Iraq: Msimamo wa Al-Afasi wafichua mtazamo wake wa kifikra na kiitikadi

14:11 - May 02, 2026
Habari ID: 3482190
IQNA – Msomaji mashuhuri wa Qur’ani Tukufu kutoka Iraq amelaani vikali misimamo ya hivi karibuni ya qari wa Kuwait, Mishary Rashid Al Afasi, inayounga mkono dhulma ya Wamarekani na Wazayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika mahojiano na IQNA, Ustadh Ali Al‑Khafaji amesisitiza kuwa misimamo ambayo Al‑Afasi amechukua ya kuunga mkono uvamizi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, zinaonyesha kuwa ameondoka katika njia ya imani na uadilifu.

Amesema: “Misimamo hii inaonyesha upeo wa fikra wa qari huyu wa Kuwait, na itikadi yake potovu ambayo kimsingi inamuumiza yeye mwenyewe."

Al‑Khafaji alitaja kitendo cha qari huyo kuwa kauli isiyo ya haki dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akiongeza:

“Kwa bahati mbaya, tumesikia kauli hii isiyo ya haki dhidi ya Iran ya Kiislamu huku taifa hilo likikabiliana na nguvu dhalimu zaidi duniani, Marekani na utawala wa Kizayuni.”

Ustadh huyo alibainisha kuwa kwa kauli hiyo, usomaji wa Al‑Afasi umegeuzwa jukwaa la kuwatetea Trump na Netanyahu dhidi ya Iran ya Kiislamu na taifa lililotukuka kwa ubinadamu, dini, na maadili.

Aidha, Al‑Khafaji alisisitiza kuwa hata katika vita dhidi ya maadui, Iran imeonyesha maadili na tabia ya Mtume Mtukufu Muhammad (SAW) na Ahlul‑Bayt (AS).

Kuhusu athari za mawazo na imani za Al‑Afasi kwa mitazamo ya umma katika ulimwengu wa Kiislamu, Al‑Khafaji alisema watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii katika nchi kadhaa za Kiarabu wamelaani na kubeza msimamo huo, wakiamini kuwa ni upotovu kutoka njia ya imani sahihi.

“Kwa bahati mbaya, Al‑Afasi amefuata itikadi potovu na atabeba madhara ya makosa yake; hivyo, kwa kitendo hiki amejiathiri mwenyewe kabla ya kuidhalilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, jambo ambalo linaonekana wazi,” alisema.

Al‑Khafaji alisisitiza umuhimu wa kuchukua msimamo wa wazi kuhusu yaliyojiri, na kumalizia kwa wito wa thabiti katika misingi ya itikadi na imani njema.

Aidha, alitaja tukio la Ibn Muljam, akieleza kuwa naye alikuwa msomaji mzuri wa Qur’ani, lakini suauti nzuri pekee haitoshi bila imani imara na ukamilifu wa kiroho.

“Wanaharakati wa Qur’ani wanapaswa kulaani na kukemea misimamo ya Al‑Afasi, kwani ni upotovu ulio wazi na ni fedheha kwake binafsi kabla ya kuwa ni tusi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,” alisema qari huyo wa Iraq.

Katika kujibu hatua za kuondoa qiraa za Al‑Afasi katika majukwaa kadhaa na kupiga marufuku kusikiliza qiraa zake, Al‑Khafaji alitangaza kuunga mkono hatua hiyo na akawataka wafuasi wa Al‑Afasi kutafakari upya ufuasi wao.

“Wasikilizaji wanaweza kuvutwa kihisia na uzuri wa sauti ya qari, wakampa heshima kubwa, ilhali mwenendo wake hutofautiana na njia ya Qur’ani,” alieleza.

4348287

Kishikizo: qari kuwait marekani iran
captcha