IQNA

Zaidi ya waumini 6,500 wa Iran wafika Madina kwa ajili ya Hija

14:45 - May 03, 2026
Habari ID: 3482196
IQNA – Afisa wa Hija kutoka Iran ametangaza kuwasili kwa zaidi ya waumini 6,500 wa Kiirani mjini Madina kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija kufikia mwisho wa usiku wa Ijumaa.

Mohammad Amin Rahmani, kiongozi wa makao makuu ya Hija ya Iran mjini Madina, amesema kuwa za kuwapokea wasafiri Wairani wanaofika Madina kwa ajili ya kujitayarisha kutekeleza ibada ya Hija mwaka hii zinaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa mipango iliyowekwa, waumini wanaotekeleza Hija mwaka huu wataendelea kuingia Madina, mji ambao ni maarufu kama Mji Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW).

Rahmani pia alitangaza kufanyika kwa mikutano kadhaa ya uratibu ikihusisha wasimamizi na maafisa wa Madina katika idara mbalimbali za viwanja vya ndege, masuala ya lishe na malazi, usafiri, n.k., ili kubadilishana mawazo na kufanya maandalizi muhimu.

Afisa huyo alibainisha kuwa idadi ya misafara inayoingia Madina kufikia mwisho wa usiku wa Ijumaa ilikuwa misafara 53 ambayo iko katika hoteli 9.

Waumini kutoka Iran wanaotekeleza ibada ya Hija mwaka huu wanaelekea nchini Saudi Arabia kutoka viwanja kadhaa vya ndege vinavyopatikana katika majimbo ya Iranya Azarbaijan Mashariki na Magharibi, Ilam, Khorasan Razavi, Khorasan Kaskazini, Khorasan Kusini, Khuzestan, Sistan na Baluchistan, Kurdistan, Golestan, pamoja na miji ya Qom na Kashan.

Mwaka huu, waumini 30,672 kutoka Iran watashiriki katika ibada ya Hija ambapo karibu 28,000 tayari wameshapitia hatua zote za kisheria na wako tayari kwa ajili ya safari hii muhimu ya kiibada katika maisha ya kila Mwislamu.

Baada ya kukaa Madina waumini wataondoka kuelekea Makka kutekeleza ibada za Hija.

3497306

Habari zinazohusiana
Kishikizo: wairani hija madina iran
captcha