IQNA

Maqari wa Qur’ani Misri Wakaribisha Kituo cha Mtandaoni cha Usomaji Qur’ani cha Al‑Azhar

14:16 - May 03, 2026
Habari ID: 3482194
IQNA – Kituo kipya cha Al‑Azhar cha kusomwa Qur’ani kwa njia ya mtandaoni, ambacho bado kiko katika siku zake za mwanzo za utendaji, kimepokelewa kwa mwitikio mpana na ushiriki mkubwa kutoka kwa maqari mashuhuri wa Qur’ani nchini Misri.

Abu Al‑Yazid Salameh, Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Qur’ani katika Al‑Azhar, amesema kuwa kituo hiki ni jukwaa la kimtandao linalounganisha asili ya usomaji wa Qur’ani na maendeleo ya teknolojia. “Kupitia jukwaa hili tunajaribu kuwapa wanaotafuta elimu pamoja na umma nafasi ya kusoma Qur’ani kwa mwongozo wa wasomaji wakubwa na wanazuoni,” alisema.

Siku ya kwanza ya shughuli za kituo hiki ilihudhuriwa na maafisa pamoja na wajumbe wa Kamati ya Marejeo ya Qur’ani ya Misri, wakiwemo Sheikh Hassan Abdul‑Nabi Al‑Iraqi, mwakilishi wa kamati hiyo; Abdel‑Karim Saleh, mwenyekiti wa kamati; na Bashir Daabs, mkuu wa kitengo cha usomaji katika Chuo cha Qur’ani cha Al‑Azhar na pia mjumbe wa Kamati ya Marejeo ya Qur’ani, kwa mujibu wa tovuti ya Cairo 24.

Katika programu hiyo, vijana kadhaa wa Al‑Azhar ambao wameifanya Misri ijulikane katika medani za kimataifa, na ambao huongoza swala katika Msikiti Mkuu wa Al‑Azhar, walisoma aya za Qur’ani. Miongoni mwao walikuwa Muhammad Ahmed Hassan, ndugu mapacha wasomaji Hassan na Hussein Hossam, pamoja na Sheikh Muhammad Ahmed Hassan.

Viongozi wa kituo hicho wamewataka wapendao Qur’ani na wanafunzi wanaotaka kunufaika na programu zijazo kujiunga na jukwaa hili la mtandaoni kwa kutembelea anwani ifuatayo: https://t.me/Azhar_Quran

3497311

Habari zinazohusiana
captcha